Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi
Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania
(UWARIDI).
Mkurugenzi
amesema kuwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na
kuenzi juhudi za kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya
lugha wa masuala ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.
Ameongeza
kuwa Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za
Sheria ya BAKITA ya mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi
karibuni ambayo itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi
hapa nchini pamoja na haki zao katika kuendeleza fani mbalimbali za
Lugha.
“Katika
azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais
wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika
hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat
Shani.
Kwa
upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika
risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya
wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha,
kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima
ya kazi zetu zote.
“Tumeamua
kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu
zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja
wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi
zao alisisitiza Bi. Matilda.
Umoja
wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa
lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na
kazi zao.
Mkurugezi
Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa
Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa
Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Rais
wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw.
Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi
wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI)
Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa
uzinduzi wa Umoja wa huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar
es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi
Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo akionesha cheti cha usajili wa Umoja wa
Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya
kuuzindua umoja huo huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es
Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi
ya wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania
(UWARIDI) wakimsikiliza mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugezi Msaidizi
Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo(hayupo pichani) katika uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa
Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi
Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamojja
na viongozi na wajumbe wa kamati kuu ya Umoja wa Waandishi wa Riwaya
wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya uzinduzi wa umoja huo katika
ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi ya vitabu vya Riwaya vilivyoandikwa na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
EmoticonEmoticon