Eneo ya fukwe ya Mnazibay
Mjini Mtwara inavyooneka kuathirika na athari za mabadiliko ya tabia
nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015 february..Naibu Waziri Mpina
Alitembelea eneo hilo kujionea athari za mabadiliko ya tabia nchi. (Picha
na Evelyn Mkokoi)
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
29/7/2016
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte
Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini mwa Tanzania,
kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara
.
Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu
tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira
kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa
na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani
hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva
na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha
kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya
nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa
kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo
hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote
inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji
wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda
hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri
afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.
Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James
Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa
kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya
hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa
baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa
baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria
ya mazingira.
Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha
Madiba na kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa
viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua
korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi
pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko
ya tabia nchi.
EmoticonEmoticon