Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi na Maafisa
Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili
Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A.
Weginah
Wakuu
wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika
mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele
cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kutoka kushoto), Mhe. Tano Mwera
(Busega),Mhe. Joseph Chilongani(Meatu), Mhe. Benson Kilangi (Itilima ) na Mhe.
Seif Shekalaghe
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (katikati) akizungumza na Viongozi na
Maafisa Kilimo wa mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini
Bariadi kikiwa na lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha
pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw.
Donatus A. Weginah na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
Katibu
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa waSimiyu, Ndg. Jeremia Shigala akichangia katika
kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya
kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu .
Viongozi
na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe.
Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa
lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani
Simiyu kwa mwaka huu.
Na Stella
Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani
humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na
Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mtaka ametoa
agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika
kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa
wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka katika wilaya zote tano za mkoa huo.
Mtaka amesema
Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki
na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa
ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza
kilimo bora na chenye tija.
“Mwaka huu
kilimo kwa mkoa wetu ni kipaumbele cha
pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya
mapato yake ya ndani, ipo haja
kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya
Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda,
Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato
katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.
Aidha, kufuatia
makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania
na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara
ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani
milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60
kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi
wanalima mazao hayo.
Katika kufikia
azma hiyo, Mtaka amewataka Maafisa kilimo kutumia muda huu kufanya tafiti
katika vituo mbalimbali vya utafiti juu
ya mbegu bora, kabla ya msimu wa mazao ya mikunde haujaanza ili wakati utakapofika
uzalishaji wa mazao hayo ufanyike kitaalam na kuongeza uzalishaji kuliko ilivyo
sasa.
Wakati huo huo
Mtaka amewaagiza viongozi na Maafisa Kilimo kutoka katika wilaya zote kuwa na
mashamba ya mifano ambayo yatatumika kama mashamba darasa kwa wananchi ili
wananchi wajifunze kutoka kwao kwa kuwaonesha kuwa maelezo wanayoyatoa
yanatekelezeka.
Kwa upande wake
Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji katika
Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Joseph Nandrie ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa
wa Simiyu kulima mazao yanayostahimili ukame kama mihogo na mtama ili
kukabiliana na baa la njaa.
Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo
EmoticonEmoticon