Mkuu
wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya
Mahale,Romanus Mkonda akitoa maelezo mafupi mbele tya waandishi wa
habari waliotembelea vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo iliyopo mkoani
Kigoma.
Mkuu
wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale
,Romanus Mkonda akizungumza na wananchama wa vikundi vya kijasiliamali
vinavyojulikana kama COCOBA vinavyosaidiwa na hifadhi hiyo (hawapo
pichani.
Baadhi
ya wanachama wa vikundi wakiwa katika mkutano na watumishi wa TANAPA
pamoja na wanahabari waliotembelea vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya
Taifa ya Mlima ya Mahale .
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA) Pascal
Shelutete akizungumza katika mkutano huo ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara
ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus
Mkonda.
Baadhi ya Wanahabari waliotembelea vijiji hivyo.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Katumbi ,Issa Zuber ,kijiji kimojawapo ambacho wanachi
wananufaika na msaada wa mafunzo ya ujasiliamali unaotolewa na TANAPA.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano ,Juma Makumbi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu
wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale
akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania ,Pascal Shelutete mara baada ya kuzungumza na wanachama wa
vikundi vinavyopewa msaada na shirika hilo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.
Wananchi
wa vijiji vya Buhungu na Konkwa vilivyoko mwambao mwa ziwa
Tanganyika wilaya Uvinza mkoani Kigoma wanalazimika kuhifadhi
mamilioni ya fedha za miradi ya vikundi vyao kwenye masanduku
ya chuma na kuyafukia chini ya ardhi kutokana na ukosefu
wa huduma za taasisi za fedha utaratibu waliodai kuwa
unaotishia usalama wa fedha hizo na pia maisha yao .
Wananchi
hao pamoja na kuwashukuru wadau wanaowasaidia likiwemo
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Hifadhi yake
ya Milima ya Mahale wamesema wanatumia njia hiyo kutokana na
kuogopa kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha umbali mrefu ili
kuzifikia taasisi za fedha zilizoko kigoma mjini na wameiomba
serikali na asasi za fedha kusogeza huduma katika maeneo ya
vijijini.
Mkufunzi
mkuu wa vikundi vya benki ya jamii ya uhifadhi (COCOBA) vinavyo
fadhiliwa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA), Simada Andrea amesema
kuwa vikundi hivyo vinavyoizunguka hifadhi ya milima ya mahale, vina
sifa za kupewa mikopo lakini benki zimekuwa zikiwakataa na kuwapa
masharti magumu.
“Sifa
za kupewa mikopo wanazo…tatizo benki zinakataa kuwakopesha kwa sababu ya
umbali, zinawataka watu wa mijini kwa madai kuwa wataweza
kuwafuatilia,” alisema.
Alisema
vikundi hivyo, vimesajiliwa na serikali za vijiji na halmashauri ya
wilaya ya uvinza iliwahi kuvikopesha kwa majaribio sh. milioni 3 na
vikarudisha kwa wakati.
“Naomba niziambie benki kuwa vikundi vya cocoba vinakopesheka na vinalipa kwa wakati,” alisema.
Hata
hivyo, Andrea aliziomba taasisi hizo za kifedha kupeleka huduma katika
maeneo yao ili ziwawezeshe kufanya shughuli zao kwa urahisi na kwa uhuru
hatua itakayowaongezea tija na ufanisi.
Naye,
afisa mtendaji wa kijiji cha Nkonkwa, Issa Fungameza alisema kuna
vikundi hivyo kwa sasa vinatunza fedha zao katika kiboksi cha chuma
kutokana na benki kuwa mbali.
“Vikundi
vinakopesheka, kwa kuwa benki ziko mbali hivyo wanashindwa kupeleka
fedha hizo benki na kuamua kuzitunza kwenye kiboksi cha chuma,” alisema.
fungameza
aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa undani zaidi kwa
kuvikopessha vikundi hivyo ili viweze kujiinua kiuchumi na kimaendeleo.
Mkuu
wa idara ya ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Romanus Mkonda
alisema TANAPA imetoa zaidi ya milioni 600 kuvisaidia vikundi
zaidi ya 70 vya wananchi katika vijiji hivyo kupata mafunzo
ya ujasiria mali , uhifadhi wa mazingira na mitaji, hatua
inayolenga kuwaepusha wananchi hao kujihusisha na uharibifu
wa mazingira na ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale
EmoticonEmoticon