MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA LEO.

June 28, 2016

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Mwenyekiti waTimu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
 Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi ya kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu yaSimba na wapenzi wa timu ya Yanga Mhe. John Kadutu akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma uliolenga kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati ambapo kamati hiyo inaratibu maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu hizo itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kukusanya madawati yatakayo pelekwa katika Halmashauri zote nchini, kushoto ni Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia Ackson akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Kuahirisha shughuli za Bunge mapema leo.
( Pichazote na Frank Mvungi-Dodoma)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »