Meneja
usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,akitoa mafunzo
kwa wanachama wa Chama cha waajiri Tanzania( ATE) wakati walipokwenda
kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama sehemu za kazi
kwenye kiwanda cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
Wanachama
wa Chama Cha Waajiri Tanzania(ATE) wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa
upishi wa TBL Group Castor Masawe, kuhusiana na uzalishaji wa bia
unavyofanyika.
Wanachama
wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya
na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba
cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
Wanachama
wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya
na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba
cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama cha Waajiri Nchini (ATE) wakiangalia vikombe vya tuzo mbalimbali ambavyo TBL Group ilishinda
………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kampuni ya TBL Group
kuonyesha mafanikio ya kuwa mwekezaji bora nchini na mchango wake
kutambuliwa na taasisi mbalimbali kwa kuitunukia tuzo ,imekuwa kivutio
kikubwa kwa taasisi zinazotaka kupata mafanikio kwa kutembelea viwanda
vyake kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu na kujua siri ya mafanikio.
Wanachama wa Chama cha Waajiri
nchini (ATE) wamefanya ziara katika kiwanda cha TBL cha Ilala ambako
wamepatiwa mafunzo ya usalama kazini ikiwemo kuona uzalishaji
unavyofanyika kiwandani hapo.
Meneja Usalama,Afya na Mazingira
wa TBL Group,Renatus Nyanda aliwapatia somo la kanuni za usalama
zinazotekelezwa na kampuni hiyo ambazo zinalenga kulinda usalama wa
wafanyakazi wanapokuwa kazini na nje ya kazi ikiwemo wageni mbalimbali
wanaofika kiwandani hapo.
Wanachama hao walifurahishwa na
mafunzo hao ikiwemo mkakati wa kampuni hiyo kuendelea kufanya uwekezaji
unaozingatia utunzaji wa mazingira,kuchangia kuendeleza uchumi wa
taifa,kupunguza tatizo la ajira na kubadilisha maisha ya jamii kuwa
bora.
EmoticonEmoticon