Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa
Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo
aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi
mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo
limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Khalifa
wa Zawiyatul lqadiria, Abas Hamdan watatu kutoka kulia akiongoza dua ya
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi
wengine wakuu wa serikali mara baada ya tukio la kukabidhi vyakula
hivyo. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa
Waziri mkuu Mama Marry Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali vya
vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry
Majaliwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vikundi vya
kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu. Tukio hilo
limefanyika katika Ofisi za Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Mlezi wa Kituo cha
Charambe Islamic Center Asile Zahali mara baada ya kukamilika zoezi la
utoaji wa vyakula mbalimbali kwa vituo vinne vya kulea watoto na watu
waishio kwenye mazingira magumu.
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry
Majaliwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa vituo hivyo kabla ya
kuwakabidhi vyakula hivyo katika Ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
MKE wa
Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati
huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea
watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es
salaam.
Vyakula
hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya Mke wa
Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500,
Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewatakia heri
Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasihi
waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.
(“Tunawatakia
mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki
tunawaomba mzidi kuiombea nchi yetu amani, viongozi wetu wa nchi na
watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na amani ndio mambo mengi mazuri
yanaweza kufanyika”)
Kwa
niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha
Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa
kutoa vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano
na ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini,
kabila wala maeneo wanayotoka.
(“Kwa
hiyo ndugu zangu mna imani ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni
ndugu zenu, wote tunajenga nyumba moja, mshikamano ndio tunu
tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa kuona wenzenu tunafanya
ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa ni ibada
kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu
hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani
nyingine, lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi
ambacho mtume wetu SWA anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata
nusura kwa wakristo”)
Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.
EmoticonEmoticon