SERENGETI BOYS WAKIWA MAZOEZINI KARUME

June 15, 2016

SER1 
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya vijana Tanzania – wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Bakari Shime akisimamia mazoezi ya viungo  kwa wachezaji wa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijiji Dar es Salaam leo Juni 15, 2016. Serengeti Boys ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Alfred Lucas wa TFF.
SER2 
Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Taifa ya vijana – Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Sebastian Nkoma na Mshauri wa Ufundi wa TFF kwa maendeleo ya timu za Vijana, Kim Poulsen wakisimamia mazoezi ya viungo kwa wachezaji wa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijiji Dar es Salaam leo Juni 15, 2016. Serengeti Boys ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Alfred Lucas wa TFF.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »