Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Angela Kairukiakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambayo
hufanyika Juni 16 -23 kila mwaka.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 23
kwa kuondoa watumishi hewa katika mfumo malipo ya mishahara ya
serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Angela Kairuki jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi
wa habari, amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana mara baada ya kuanza
kwa kutafuta watumishi hewa wa serikali.
Amesema
kuwa watumishi ambao wameshaondolewa tangu Machi, 1 hadi Mai 30 ni
watumishi 12,246 ameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya
Serikali kwa sababu mbalimbali ikimo kutimiza umri wa Kustaafu kwa
lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kuhitimishwa kwa mikataba.
Aidha amesema kuwa wasingeondolewa kwenye mfumo wa mishara kwa wafanyakazi wa serikali zaidi ya shilini Bilioni 25 zingepotea.
EmoticonEmoticon