Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili
kushoto), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bw.
Gishuli Charles (wa nne kushoto), wakati alipoanza ziara yake ya ukaguzi
wa miundombinu katika Mkoa wa Singida. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard
Chimagu, na wa tatu kushoto ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Eng.
Leonard Kapongo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard
Kapongo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.
Makame Mbarawa uharibifu wa barabara unaotokana na ajali za barabarani
katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilometa 89.3
mkoani Singida.
Wananchi
wa Itigi wakimsilikiza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.
Makame Mbarawa, (hayupo pichani) alipotangaza kuanza kwa ujenzi wa
barabara ya Mkiwa-Itigi-Makongorosi kwa kiwango cha lami itakayoanza
kujengwa kwa kilomita 35 mkoani Singida.
Meneja
wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Singida Eng. Leonard
Kapongo (wa tano kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto) kuhusu mradi wa
ujenzi wa mzani katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambao ujenzi
utakamilika hivi karibuni.
Muonekano wa ujenzi wa kituo cha Mzani Itigi, kinachojengwa katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, mkoani Singida.
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akionesha moja
ya picha ya uharibifu wa alama za barabarani uliofanywa na wananchi
katika ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita
89.3.
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akihutubia
wananchi wa Itigi mara baada ya kukagua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya
yenye urefu wa Kilomita 89.3 mkoani Singida, ambayo ujenzi wake kwa
kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 98.
Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisalimiana
na wananchi wa Itigi mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Katikati ni Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare.
Muonekano
wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3
inayojengwa na Mkandarasi SynoHydro Corporation Limited kutoka China
inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 109 mkoani Singida.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
EmoticonEmoticon