Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua madawati hayo kabla ya kuyagawa.
Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla akigawa madawati hayo.
Halmashauri
ya Mbeya imekamilisha utengenezaji wa madawati 5,371 ikiwa ni agizo la
Rais kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa katika madawati.
Akisema
taarifa kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Upendo Sanga amesema wamekamilisha maoema utengenezaji
madawati mapema kabla ya juni 30 kwenda sambamba na agizo la Mkuu wa
mkoa halmashauri zote zikamilishe madawati tarehe 20 juni siku kumi
kabla ya tarehe ya mwisho ya mheshimiwa Rais.
Mkuu wa Mkoa amekabidhi madawati 3,746 kwa shule 51 na yaliyobaki ameagiza yaendelee kukabidhiwa kwa Shule zingine.
Amesisitiza halmashauri zote kukamilisha utengenezaji wa madawati ifikapo tarehe 20 Juni.
EmoticonEmoticon