Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (katikati) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya
Tanzania na Zambia, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa
mazao ya misitu hususan magogo katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wanaoshuhudia kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili, Gladynes Mkamba na
Kaimu Mtendaji Mkuu TFS, Richard Kamwenda (kushoto). Waliosimama kulia ni
Mwanasheria wa TFS, David Mung’ong’o na Mwanasheria wa Wizara ya Maliasili, Stephen
Mwamasenjele.
Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia,
Trevor Kaunda akisaini makubaliano hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakibadilishana hati ya makubaliano
waliyosaini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao
ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi hizo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla fupi ya kuweka makubaliano
kati ya Serikali
ya Tanzania na Zambia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na
changamoto za udhibiti wa
usafirishaji wa mazao ya misitu hususani magogo katika mipaka ya nchi
hizo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Maliasili na Hifadhi ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda.
Maj. Gen. Milanzi alisema kuwa ushirikiano huo utaleta tija katika
udhibiti wa biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo kutoka
katika nchi hizo kwenda nchi nyingine kupitia mipaka ya nchi hizo na
bandari ya Dar es Salaam. Aliwataka watanzania wanaojihusisha na
biashara haramu ya uvunaji na usafirishaji wa magogo nje ya nchi waache
mara moja kwani Serikali imejipanga kuhakikisha wanakamatwa na sheria
kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiteta jambo wakati
wakikagua Makontena 103 ya magogo (nyuma pichani) yaliyokamatwa hivi karibuni
katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao
wamesaini makubaliano ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji
wa mazao ya misitu hususani magogo kwenye mipaka wa nchi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maliasili na Hifadhi
ya Mazingira wa Serikali ya Zambia, Trevor Kaunda wakiangalia sehemu ya magogo
yaliyokamatwa hivi karibuni katika bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini
Zambia na DRC. Makatibu Wakuu hao wamesaini makubaliano ya kukabiliana na
changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususani
magogo kwenye mipaka wa nchi hizo. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)
EmoticonEmoticon