Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Bw. Nehemia Murusuri, Bi. Getrude Lyatuu na Bi. Awa Dabo, walipomtembelea Naibu Waziri Mh. Luhaga Mpina hii leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya mazungumzo baina yao.
Na Lulu Mussa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga
Mpina hii leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo pamoja na ujumbe
aliombatana nao, Ofisini kwake Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao ujumbe huo umeonyesha nia ya kufanya kazi kwa
karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais hususan katika nyanja ya Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya
Tabianchi na nishati mbadala.
Awali Naibu Waziri Mpina aliwafahamisha kuwa Ofisi yake imeandaa Mpango
Mkakati wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima na kuwataka wadau wa maendeleo
kuwaunga mkono. "Tunaendelea na jitihada za kupanda Miti mingi
iwezekanavyo na katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa
ajili ya kazi hiyo" alisisitiza Naibu Waziri Mpina.
Aidha, Naibu Waziri Mpina ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo
kujitokeza kuunga mkono kampeni hii kubwa ya upandaji miti nchi nzima
na kusisitiza kuwa uhai wa viumbe vyote unategema Mazingira hivyo ni
vema kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mheshimiwa Mpina pia amesema Ofisi yake kwa sasa inafanya marekebisho
ya Sera ya Mazingira na kujenga uwezo kwa watendaji wa ngazi zote juu
ya kusimamia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 pamoja na kuelimisha
Umma juu ya kampeni ya Usafi ya kila mwisho mwa mwezi.
kwa upande wake Bi. Dabo amesema kuwa shirika lake limeweka vipaumbele
vya kutekeleza ndani ya miaka mitano ambavyo vinaendana na Mpango wa
Maendeleo wa Taifa, sambamba na kusaidia vikundi mbalimbali katika ngazi
za vijiji juu ya kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.
Bi Dabo ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika jitihada
za kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.
EmoticonEmoticon