Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ leo Mei 17, 2016 imechanua vema baada ya kuilaza India
mabao 3-1 katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa
iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India katika mchezo huo uliofanyika
Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India.
Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani katika dakika ya
21 wakati lile la pili India walijifunga baada ya beki wake kuhangaika
kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28 wakati lile la tatu
lilifungwa na Asad Juma katika dakika ya 48 huku lile la India
likifungwa na Komal Thatal katika dakika ya 38.
Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa wanasubiri angalau sare au
ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini
utakaopigwa Alhamisi Mei 19, 2016 na Malaysia Mei 21, 2016 ili icheze
nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Mei 12 kabla ya kufikia fainali
zake Mei 26, mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoka
sare ya Marekani ya bao 1-1.
Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliwakilishwa na Ramadhani Kabwili,
Ally Nganzi, Ally Msengi, Asad Juma, Dickson Job, Issa Makamba, Maziku
Amani, Nickson Kibabage, Shaaban Ada, Syprian Mtesigwa na Mohammed
Abdallah.
India: Mohammed Nawaz, Reamsochung Aimol, Boris Singh, Mohammed
Khan, Juendra Singh, Suresh Wangjam, Amarjit Kiyam, Khumanthem Meetei,
Sandjev Staldi, Aniket Jadhav na Komal Thatal.
Matokeo haya yanapatikana pia kupitia link za:
Indian Football Team Official FB page: https://www.facebook.com/TheIndianFootballTeam/
AIFF Youtube channel: https://www.youtube.com/channel/UCiZ7OnWhEiPMA3II0VgLA6A
EmoticonEmoticon