Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.
Rai
hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa
mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari
ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule
hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza
kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.
Dk.
Kigwangalla amewapongeza wanafunzi hao 136 ambapo kati yao wanafunzi
80, ni wa mchepuo wa Sayansi ambapo amewataka kuto kata tamaa na baadala
yake waongeze juhudi hadi elimu ya juu Zaidi ya ngazi ya Chuo huku pia
akiwataka wanafunzi wengine hapa nchini kujikita katika masomo hayo ya
Sayansi katika zama za sasa ambayo Tanzania inaelekea katika mapinduzi
ya viwanda na uchumi wa Kati.
“Nina
Imani na nyie. Najua hamta niangusha na mutafaulu vizuri. Nawapongeza
wanafunzi wote wanaohitimu leo hii. Ni imani yangu kuwa nyote mtafaulu
vizuri sana katika mitihani yenu ya kidato cha Sita kwa kupata daraja la
kwanza (Division I) na wachache sana daraja la pili (Division II). Sina
mashaka, najua mtailetea shule yenu (Mazinde Juu) heshima kubwa ndani
na nje ya nchi” alibainisha Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hutuba
maalum ya maafali hayo.
Dk.
Kigwangalla aliongeza kuwa, katika hali ya sasa ya soko la ajira kuwa
gumu, aliwataka wanafunzi hao kuzingatia kipindi hiki kifupi cha kuwa
nyumbani na baadae kusubiria masomo ya elimu ya juu ya ngazi ya Chuo,
kuwa watakutana na vizingiti mbalimbali hivyo amewataka kuzingatia
uadilifu walioupata shuleni hapo.
“Ndugu
zangu wahitimu, ni kweli kwamba nchi yenu ina changamoto ya ajira.
Wasomi ni wengi lakini kazi hakuna. Kwenu ninyi tayari mna sifa kwani
mnaonekana mna tabia nzuri. Pia matumaini ya kufanya vizuri kwenye
mtihani wenu wa taifa. Cha maana endeleeni kuwa waadilifu na chuoni
mkasome bidii. Serikali inahangaika na kazi zitaendelea kupatikana tu.
Aidha,
Dk. Kigwangalla alipongeza uongozi wa shule na bodi inayosimamia shule
pamoja na wazazi kwa kuwezesha shule hiyo kuifikisha hapo ilipo ikiwemo
katika mafanikio ya kielimu kwa wanafunzi wanaopitia shule tokea
ilipoanzishwa kwake.
Kwa
upande wake Mkuu wa shule hiyo, Sister Evetha Kilamba ameipongeza
Serikali kwa ushirikiano wanaotoa kwa Shule mbalimbali hapa Nchini
ikiwemo shule hiyo ambapo pia alimpongeza Mgeni rasmi Dk. Kigwangalla
kwa kuwezesha kuongeza hamasa kwa shule hiyo ikiwemo harambee
iliyoendeshwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Walimu shuleni hapo.
Naye
Mbunge wa Lishoto, Mh. Shabani Omari Shekilindi alitoa wito kwa
wanafunzi hao kuzingatia maadili mema nje ya shule na kujiandaa na
elimu ya Chuo huku akiwataka kuzingatia suala la elimu katika maisha
yao.
Wanafunzi hao wa kidato cha Sita wakimshangilia mwalimu wao Mkuu wakati wa mahafali hayo
Mwenyekiti
wa Bodi ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Ndugu Elishilia Kaaya
akitoa maelezo machache namna wanavyoendesha shule hiyo pamoja na
kuwahusia wanafunzi hao wanaohitimu
Burudani ikiendelea katika mahafali hayo.. ya kidato cha sita, St. Mary's Mazinde Juu
Bango
la kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita kama linavyoonekana na kusomeka
ambapo burudani iliandaliwa na wanafunzi wanaoingia kidato cha sita wa
shule hiyo
Wanafunzi wa wahitimu wakitoa hutuba yao pamoja na kuaga shuleni hapo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika mahafali hayo huku akitoa
msisitizo juu ya wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi kwa ukuaji wa
uchumi
Dada Mkuu wa shule ya St. Mary Mazinde Juu akiwasha mshumaa kuashiria kwa kufunguliwa tafrija hiyo upande wa keki.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akiendesha harambee maalum ya kuchangia ujenzi wa
nyumba za walimu. Wengine ni Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari
Shekilindi (kushoto) na kulia ni Mama Amina Shamdasi ( mzazi Rasmi)
Dada Mkuu wa kwanza wa shule hiyo (Head Girl) akitoa nasaha zake kwa wanafunzi hao wanaohitimu
Mmoja
wa wazazi akitoa shukrani zake katika tukio hilo. Mzazi huyo ni
miongoni mwa waliojenga shule hiyo ambapo ilielezwa kuwa alichangia
matofali na shughuli zingine wakati wa ujenzi wa shule hiyo wakati
inaanzishwa.
Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari Shekilindi akitoa shukrani zake..
Wazazi wakilishwa keki na watoto wao katika tukio hilo
Mbunge wa Lushoto Mh. Shabani Omari Shekilindi akimlisha keki binti yake ambaye amemaliza katika shule hiyo.
Wazazi wakiwalishwa keki na wanafunzi hao
EmoticonEmoticon