Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.
Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.
Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.
Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza)
HOTUBA YA MGENI RASMI, KWENYE UZINDUZI WA MRADI WA
UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA KATIKA MKOA WA MWANZA
APRILI 27, 2016
Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa,
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya,
Ndugu Kiongozi wa Timu ya Mradi,
Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mwanza,
Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri,
Ndugu Wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa,
Ndugu Wakurugenzi
wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Ndugu Wataalam kutoka TAMISEMI na Taasisi zingine
za Serikali,
Ndugu Watendaji
wa Mashirika na Taasisi za Umma na Binafsi,
Ndugu Wakuu wa Idara kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Ndugu wana Habari,
Ndugu Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote, napenda
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sisi sote afya njema na kutuwezesha
kufika mahali hapa salama. Aidha, napenda
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Sekretarieti
ya Mkoa na Timu ya Mradi wa Uimarishaji
Mifumo ya Sekta za Umma kwa maandalizi mazuri ya Mkutano huu wa uzinduzi wa
Mradi. Nawashukuru Wageni waalikwa wote kwa kukubali mwaliko wa kushiriki
katika Mkutano huu muhimu.
Binafsi nimefarijika sana kwa kunipa heshima kubwa
ya kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi huu wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta
za Umma “Public Sector Systems
Strengthening (PS3)” kwa mkoa wa Mwanza.
Ndugu Washiriki,
Mkoa wa Mwanza umekuwa na bahati kubwa ya kuwa
mmoja kati ya Mikoa 13 hapa nchini ambayo itafaidika na mradi huu. Ninafahamu kwamba mradi huu umezinduliwa
katika Mikoa ya Iringa, Shinyanga, Dodoma, na Morogoro. Nimeambiwa hivi sasa Mkoa
wa Mwanza unafanya uzinduzi sambamba na Mikoa ya Mbeya na Mtwara. Natoa
shukrani zangu za dhati kwa Watu wa Marekani ambao ndiyo wafadhili wa Mradi
huu, kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Ndugu Washiriki,
Mradi huu wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma
umeanza kwa wakati muafaka. Kama mnavyofahamu, tayari kuna juhudi kubwa
zinazoendelea kufanywa na Serikali yetu chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Juhudi hizi zinadhihirisha kwamba
serikali ina dhamira njema ya kuhakikisha inawahudumia wananchi ipasavyo, na
kwamba mifumo iliyopo Serikalini inakuwa na Tija kwa ajili ya kumsaidia
mwananchi katika Taifa letu.
Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani kwa
ari kubwa ya kuchapa kazi na juhudi kubwa zimekuwa zikifanyika katika
kurekebisha mifumo tuliyo nayo hivi sasa.
Ni imani yangu kuwa Mradi huu utakuwa tija kwa utoaji wa huduma bora za
Serikali kwa wananchi.
Leo tumejumuika pamoja na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya na Watendaji
mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, hii ni ishara kubwa kuonesha kuwa kazi ambayo Mradi huu unalenga kufanya
ni kubwa na muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Mkoa wetu wa Mwanza na Taifa kwa
ujumla. Ni vizuri tukatambua umuhimu huo na kushirikiana kikamilifu na Wataalam
wa mradi ili kuhakikisha kwamba lengo lililokusudiwa linafikiwa.
Ndugu Washiriki,
Kuanzia miaka ya 1990, Serikali ilikuwa
ikitekeleza Maboresho katika Sekta ya Utumishi wa Umma kwa awamu mbalimbali, na
katika awamu hizo, moja ya maboresho ambayo Serikali ilitekeleza ilikuwa ni
Mpango wa Kurekebisha Utumishi Serikalini (Civil
Service Reform Programme). Baadhi ya
mambo muhimu yaliyokuwepo kwenye mpango huo ni kuweka utaratibu ambao ungeondoa
wizi wa fedha za Umma uliokuwa ukifanywa kwa njia mbalimbali kama vile kuwepo
kwa Watumishi hewa.
Chini ya Programu hiyo ya kuboresha Utumishi wa
Sekta za Umma, Serikali imeweka Mifumo ya Kimenejimenti kwa kusaidia kuongeza
uwajibikaji katika shughuli za Serikali. Maeneo ambayo yamekuwa
yakishughulikiwa, ni pamoja na uwekaji Muundo mpya wa Utumishi wa Umma,
Uboreshaji utendaji kazi, Uboreshaji maslahi ya Watumishi, na Uboreshaji mifumo
ya kumbukumbu, Nyaraka na taarifa za watumishi. Pia eneo lingine muhimu
lililoangaliwa ni la kujengea watumishi uwezo zaidi katika kutekeleza majukumu
yao ya kazi.
Ndugu washiriki,
Serikali imeanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(BRN) ambao unalenga kutoa msukumo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali
tuliyojiwekea kwa ufanisi mkubwa zaidi. Moja ya mambo yanayozungumzwa kwenye Mpango
huu ni kuimarisha mifumo kwa sababu bila mifumo imara utekelezwaji wa kazi
tulizojipangia hauwezi kufanikiwa.
Kwa wale wafuatiliaji wa mambo yanayoendela hapa
nchini, mtakumbuka kwamba wakati Waheshimiwa Wakuu wapya wa Mikoa tulipokuwa tunaapishwa,
Mhe. Rais alitupa agizo la kuhakikisha Watumishi hewa wote wanaondolewa kwenye
Ankara za Mishahara ndani ya siku kumi na Tano (15). Hii inaonyesha namna tatizo lilivyo
kubwa, na namna serikali ilivyokusudia kuliondoa kabisa. Jambo hili lazima
litekelezwe, na huu ndiyo Uimarishaji wa
mifumo yenyewe.
Ndugu Washiriki,
Ni muhimu tukumbuke kwamba upatikanaji wa Huduma Bora
za Serikali ni haki ya kila raia wa nchi hii. Hata hivyo, ili tuweze kutekeleza
kazi za Serikali za kuhudumia Wananchi kwa ufanisi, ni lazima tuwe na mifumo
imara. Nimeambiwa kuwa Mradi huu unaouzinduliwa leo katika Mkoa wa Mwanza
utashirikiana na Serikali na Sekta nyingine katika maeneo ya Utawala Bora na
Ushirikishwaji wa Raia, Rasilimali watu, Fedha, Mifumo ya Mawasiliano, na
Tafiti Tendaji. Haya ni maeneo muhimu
ambayo bila shaka yatazipa Halmashauri zetu uwezo wa kumhudumia mwananchi kwa
ufanisi zaidi.
Uwepo wenu Watendaji wa ngazi ya Mkoa na Halmashaurini
muhimu sana katika uzinduzi huu, kwa sababu ninyi ndio mnaotegemewa kutekeleza
shughuli za Serikali katika maeneo yenu, na ndio wenye mawasiliano ya moja kwa
moja na wananchi wa kawaida.
Napenda kutoa Rai kwa Watendaji wote wa ngazi ya Mkoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa mnatoa ushirikiano wa kutosha kwa
kufanya kazi bega kwa bega na wataalam wanaoendesha Mradi huu wa Uboreshaji
Mifumo ya Sekta za Umma. Kwa kutambua na kufahamu kwamba mradi huu ni wa kwetu
kwa manufaa ya nchi yetu, hivyo uwajibikaji ni muhimu ili kuhakikisha kwamba
mradi huu unakuwa na mafanikio makubwa.
Ndugu Washiriki,
Sisi sote tuliopo mahali hapa tunao wajibu wa
kuitekeleza Falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’
kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba mifumo tuliyo nayo inaboreshwa na mradi huu
unafanikiwa kikamilifu. Ni matumaini yangu kuwa katika siku mtakazo kuwa hapa
kujadiliana namna ya kutekeleza Mradi huu katika Halmashauri zenu, mtaandaa Mpango
Kazi wa utekelezaji wa shughulina kuainisha maeneo ya vipaumbele ambayo mna
uhakika kwamba ndiyo yenye tija katika kutekeleza Mradi huu kwa ushirikiano.
Mwisho, napenda tena kutoa shukrani zangu za dhati kwa
timu ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa utayari wao wa
kuusaidia Mkoa wetu katika Mradi huu na Watu wa Marekani kupitia Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Karibuni sana katika Mkoa wa Mwanza.
Baada ya
maelezo haya, sasa napenda kutamka kwamba Mradi huu wa Uimarishaji wa Mifumo ya
Sekta za Umma umezinduliwa Rasmi Mkoani Mwanza.
ASANTENI SANA
KWA KUNISIKILIZA
EmoticonEmoticon