LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA JUMATANO

April 03, 2016
Mchezo kati ya Young African dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Jumatano ya April 6, 2016 umesogezwa mbele na sasa utachezwa tarehe 16 Aprili 2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Jumatano ya Aprili 6, ligi kuu itaendelea kwa michezo miwili tu, Azam FC watakua wenyeji wa Ndanda FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, huku Majimaji FC wakiwakaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Majimaji Songea.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »