Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt. JOHN MAGUFULI wilayani CHATO

April 02, 2016
. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasili
kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kwenda
kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 
………………………
Waziri Mkuu
Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni
katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
 
Mheshimiwa Odinga
ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga,
wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02
April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais
Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe
Mama Janeth Magufuli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake
Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana na
Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada ya kuwasili nyumbani
kwake Chato Mkoani Geita.
 
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
 
“Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato” Alisema Mheshimiwa Odinga.
 
 
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais
John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga
Bi. Ida Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani
Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na
mama mzazi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara
baada ya kuwasili Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyepo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
“Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato” Alisema Mheshimiwa Odinga.
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama Mzazi wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
02 April, 2016

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »