WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ATETA NA WAFANYABIASHARA MKOA WA ARUSHA,WAAHIDI KUUNGA MKONO SERIKALI

February 26, 2016

 
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango akizungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Arusha leo katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa na kuwakumbusha wajibu wao kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu na Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja.
Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja akijibu hoja za wafanyabiashara mkoa wa Arusha huku Waziri wa Fedha na Mipango,Philip Mpango akifatilia kwa makini . 
Mfanyabiashara wa Usafirishaji ambaye ni Katibu wa Wamiliki wa magari ya abiria mkoa wa Arusha na Kilimanjaro(AKIBOA)Roken Adolf akiuliza maswali na kutoa maoni ya wanachama wenzake.
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha nguo na bidhaa mbalimbali cha A to Z,Anuj Shah akizungumza namna mlolongo wa nyingi unavyowakera wawekezaji wa ndani.
Mkurugeni wa taasisi kilele inayohusika na kilimo cha mbogamboga na matunda ya TAHA,Jackline Mkindi aliiomba serikali kuweka mazingira mazuri na kupunguza kodi ili kuwezesha ndege za mizigo kutoa huduma zao hapa nchi badala ya kusafirisha mazao yao kupitia nchi ya Kenya.
Mkurugenzi wa Kibo Guides and Tanganyika Wildernes Camps akizungumza kwenye mkutano huo ambao aliiomba serikali kuwabana wafanyabiashara wa utalii wanaokwepa kodi.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Ernest Kahindi,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Francis Miti na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Omary Kwaang’ wakifatilia miongoni mwa maafisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo.
Wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali waliohudhudia mkutano huo
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com,Arusha

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »