Waziri Mkuu Mhe. Kassimu
Majaliwa,Majaliwa akizungumza na mawaziri na manaibu waziri wakati wa
semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu
Jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
Waziri ofisi ya Rais Utumishi na
Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza wakati wa semina ya
Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es
salaam.
Kamishna Tume ya Maadili kwa
viongozi wa Umma Jaji Mstaafu salome Kaganda akizungumza wakati wa
semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu
Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mawaziri na manaibu
Waziri wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda ikiwa ni ishara ya kuonesha
uzalendo kwa nchi kabla ya kuanza semina ya Maadili kwa mawaziri na
manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini
Bi Virginia Blaser akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii
Mh. Profesa Jumanne Maghembe huku mawazili wengine wakisililiza
mazungumzo hayo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimsikiliza Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. JumanneMaghembe kabla ya kuanza kwa semina ya
Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es
salaam katikati ni Waziri ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage
Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza jambo
pamoja na mawaziri wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo semina ya Maadili
kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam
,kulia ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Uratibu, Bunge,Ajira na
Walemavu Mhe. Jenista Muhagama(Kulia na katikati ni Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi.
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani
Mh. Hamad Masauni kushoto akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ofisi
ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina huku mawazili wengine
wakupitia makabrasha yao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo kwa mawaziri na manaibu
iliyotolewa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewaasa Mawaziri na Manaibu
Waziri kuzingatia sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma
kwani maadili ni nyenzo kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimi wa Majaliwa ameyasema
hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya
Maadili kwa Mawaziri na Manaibu Waziri inayolenga kuwajengea uwezo
mkubwa yanamna kiongozi wa utumishi wa umma anavyotakiwa kutekeleza
majukumu yake bila kukiuka maadili.
“Chimbuko la Maadili ya Utumishi
wa Umma ulianza tangu siku nyingi na umekuwa ukitajwa katika sehemu
mbalimbali ikiwemo katika Katiba ya nchi ya mwaka 1977, Sheria za
Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishiwa Umma,”alisemaMajaliwa.
Akiendelea kuzungumza katika
Semina hiyo WaziriMkuu alisisitiza kuwa Semina hiyo siyo semina elekezi
kwa viongozi hao kama jinsi imekuwa ikijadiliwa katika mitandao ya
kijamii, bali ni semina inayolenga kutoa mwongozo wa maadili ya viongozi
wa umma na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya Uadilifu na mada katika
semina hiyo zitahusu masuala ya maadili tuu.
Kwa upande wa Kamishna wa Maadili
Jaji Mstaafu Salome Kaganda kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya
Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma amesema semina ya maaadili kwa
viongozi ni jukumu la Sekretariati ya maadili kuandaa kwani hiyo ni
sehemu ya majukumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Utumishi wa Umma na wao ndiyo wenye wajibu wakuhakikisha viongozi wa
utumishi wa umma wanazingatia maadili.
“Sekretarieti ya Maadili kwa
Viongozi wa Utumishi wa Umma inamamlaka ya kufanya uchunguzi kwa
kiongozi yoyote wa umma atakayesikika kukiuka maadili kama kiapo cha
ahadi za uadilifu kinavyosema,”alisema Jaji Mstaafu Salome.
Aidha Kamishna wa Maadili huyo
aliendelea kusema Ofisi ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa
Utumishi wa Umma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
rasimali fedha ambapo wanazaidi ya miaka mitatu wameshindwa kufanya
uhakiki wa mali za viongozi pamoja na uchunguzi kutokana na changamoto
hiyo.
Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi
ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma kwa
kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na Shirika la USAID.
EmoticonEmoticon