MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amezindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future)
ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi
na makampuni mbalimbali.
Uzinduzi huo uliofanyika leo katika Hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na watu
mbalimbali wakiwepo wakenya, waganda na watanzania na watu kutoka bara
la Ulaya na Asia.
Makamu
wa Rais, Samia Suluhu amesema kuwa wanawake ni watendaji wazuri na
wanamaamuzi mazuri katika uongozi na uendelezaji wa makamuni pamoja na
Tasisi mbalimbali.
Mpango
huo uliozinduliwa leo umefanywa wanachana chama cha waajili Tanzania
ambao unalenga kuwajengea uwezo wanawake ili kuongeza ufanisi katika
biashara zao na kujenga mtandao ambao utaongeza juhudi na maarifa kwa
wanawake.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza wakati wa kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati
ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za
wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika
ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
Mwenyekiti wa kampuni ya ATE, Zuhura Muro akizungumza na wanawake
kutoka kutoka makampuni mbalimbali leo wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua mpango malumu
wa kuwafundisha wanawake ili waweze kuwa na uwezo wa kuleta mawazo
yenye kuinua kampuni au taasisi mbalimbali kuwa kubwa.
Mtumbuizaji
akitumbuiza katika uzinduzi wa mpango wa kuinua wanawake katika uongozi
wa juu katika makampuni au taasisi mbalimbali, uzinduzi huo umefanyika
leo katika hoteli Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akitoa ushuhuda alioufanya
katika taasisi hiyo ya fedha kwa maendeleo ya wanawake waliokusanyika
leo ili kuzindua mpango wa kuwaundisha wanawake uongozi katika makampuni
na Tasisi mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama akizungumza leo katika uzinduzi wa Programe
maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea
uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni
mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam leo.
Wadau
mbalimbali wakisikiliza shuhuda mbalimbali za wadau wa uongozi kwa
wanawake kutoka hapa nchini, Uganda na Kenya leo katika uzinduzi wa Programe
maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea
uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni
mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama leo katika uzinduzi
wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) amayo
itawajengea uwezo wanawake katika uongozi wa juu wa taasisi na makampuni
mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Programe maalum ya
Mwanamke na wakati ujao (Female Future) katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
EmoticonEmoticon