Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole
waathirika wa mafuriko wa kata ya Mapogolo tarafa ya Idodi wilaya ya
Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada wa pesa zaidi ya Tsh
milioni 9 kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbali mbali ikiwa ni pamoja
na kurejesha miundo mbinu ya maji safi iliyoharibiwa na mafuriko.
Bw Lukuvi ambae pia ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo
ya makazi alikabidhi msaada huo jana baada ya kutembelea waathirika
hao waliopo kambi ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara
ya kutoka Iringa kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo kwa sasa
imekarabatiwa baada ya awali barabara hiyo kukatika kutokana na
mafuriko hayo , alisema kuwa lengo lake kama mbunge wa jimbo
hilo la Isimani na serikali ni kuona wananchi waliokumbwa na mafuriko
wanaendelea kusaidiwa .
Mbunge wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa
Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti
wa kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 2
za kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishiwa makazi mapya
kutoka kitongoji cha Kitanewa Idodi ambao nyumba zao zilisombwa na
mafuriko.
Alisema kuwa awali aliomba msaada wa mahindi tani 100 kutoka
serikali kwa ajili ya waathirika hao wa mafuriko Idodi na Pawaga
ikiwa ni pamoja na kuwasaidia msaada wa fedha kiasi cha zaidi
ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya kuwawezesha waathirika hao wa mafuriko
kupata mahitaji mengine kama mboga na pesa ya kusagia mahindi hayo .
Bw Lukuvi alisema kuwa kwa ajili ya kurejesha huduma ya maji
kijijini hapo amewasaidia kiasi cha Tsh miliobni 4 ambazo wameomba
kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2
kwa ajili ya kukiwezesha kijiji kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi
waliotoa ardhi yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha Kitanewa ambao
wanapaswa kuhamishwa eneo hilo la mafuriko la kupewa makazi mapya .
Wananchi wanaotakiwa kuhamishwa kwenda makazi mapya baada ya
nyumba zao kusombwa na mafuriko wakimsikiliza kwa makini mbunge wao
Lukuvi.
" Waambieni watu wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili
ya viwanja mwaka huu wavune mazao yao na baada ya hapo kila mmoja
muweze kumlipa fidia ya Tsh 200,000 na baada ya hapo waitini
wataalamu wa ardhi ili waweze kupima viwanja na mpanfgilio mzuri
zaidi kwa ajili ya makazi mapya .......pia nataka hata mashamba ya
kawaida ya wananchi kupimwa ili kupata hati za ardhi zitakazowawezesha
kutumia kupata mikopo ....ila nitawaletea mashine za kufyatulia
tofari ambazo unaweza kuzijengea bila kuchoma "
Alisema kuwa kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora
mwananchi atakayekuwa wa kwanza kupandisha jengo atamchangia bati
japo kwa sasa amekwisha toa bati zaidi ya 300 kwa mkuu wa wilaya ya
Iringa kwa ajili ya waathirika hao.
Lukuvi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katikati jana.
Bw Lukuvi pia amewapongeza wadau mbali mbali zikiwemo taasisi
za dini ,watu binafsi ,taasisi ya kifedha pamoja na mifuko ya
hifadhi za jamii kwa kujitolea misaada mbali mbali kwa ajili ya
waathirika wa mafuriko na wagonjwa wa Kipindupindu Pawaga .
Pamoja na kuwashukuru wadau hao Lukuvi alimpongeza waziri
Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwatembelea waathirika hao wa Mafuriko na
wale wa Kipindupindu Pawaga .
Hata hivyo Lukuvi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw
Richard Kasesela na viongozi wote akiwemo mkuu wa mkoa Amina Masenza
kwa kusimamia shughuli mbali mbali ikiwemo ya urejeshaji wa miundo
mbinu ya barabara iliyokuwa imekatika katika barabara ya Iringa -
Ruaha .
Katika hatua nyingine Bw Lukuvi aliagiza serikali ya kijiji
cha Mapogolo kutowabagua wananchi katika kugawa chakula hicho cha
msaada na kutaka hata ambao si waathirika wa mafuriko ambao wana
njaa wapewe chakula hicho cha msaada kwa waathirika wa mafuriko .
Wakati huo huo Waziri Lukuvi alisema kuwa serikali inakusudia
kuijenga barabara ya Iringa- kuelekea hifadhi ya Ruaha kwa kiwango
cha lami kama mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati wa
kampeni kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM
Pia kwa ajili ya kuwafanya wananchi kunufaika watalii
wanaotembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa alisema tayari jitihada za
kujenga viwanja vidogo vya ndege nje ya hifadhi ya Ruaha zimeanza
na kuwa lengo la serikali ni kuwahamisha wafanyakazi wanaoishi
ndani ya hifadhi hiyo na kujumuika na wananchi nje ya hifadhi ili
waweze kupata mahitaji kama wananchi wengine.
Mmoja
kati ya wakazi wa KItanewa ambao walikubwa na mafuriko aliyepata kusoma
na waziri Lukuvi darasa moja shule ya msingi akimsikiliza mbunge wake
Lukuvi akitoa maelekezo kwa wananchi wa Kitanewa Idodi.
Mkazi wa Kitanewa akilalamika kunyimwa msaada wa mahindi ya msaada
wakati yeye ni mlemavu japo si mlengwa wa msaada huo wa waathirika wa
mafuriko
Lukuvi akielezwa jambo na mmoja kati ya waathirika wa mafuriko Idodi.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimweleza jambo mbunge Lukuvi
MKazi wa kitanewa Idodi akimpongeza mbunge wake Lukuvi kwa kuwajali wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Katikati na kamati yake
ya Ulinzi na usalama wakitazama daraja la Iringa -kuelekea hifadhi ya
Ruaha ambalo awali lilikuwa halipitiki baada ya kusombwa na mafuriko na
sasa linapitika.
EmoticonEmoticon