Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) imeendelea leo jumamosi kwa michezo mitano huku
mchezo ulivuta hisia za mashabiki wengi wa soka ukiwa ni pambano la
watani wa jadi Yanga na Simba.
Katika
mchezo huo ambao Yanga ilikuwa wenyeji umemalizika kwa Yanga kuendeleza
ubabe kwa watani zao Simba baada ya kuwafunga goli mbili kwa bila na
huku ikikumbukwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliibuka na
ushindi sawa na ushindi wa leo.
Mchezo
ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku Simba ikionekana
kujisahau kwa kucheza faulo nyingi karibu na maeneo ya lango lao nao
Yanga wakionekana kuwa wajanja kwa kutengeneza ukuta imara ambao
washambuliaji wa Simba walishindwa kuupita.
Katika
dakika ya 25, beki wa Simba, Abdi Banda alionyeshwa kadi nyekundu na
mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa baada ya kuonyeshwa kadi ya pili
ya njano kwa kumchezea faulo mshambualiji wa Yanga, Donald Ngoma.
Dakika
10 mbele baada ya Banda kuonyeshwa kadi nyekundu, Yanga ilifanikiwa
kupata goli kupitia kwa Donald Ngoma baada ya beki Hassan Kessy
kurudisha mpira ambao hakuupiga kwa kasi kwa golikipa wa Simba, Angban
na ndipo Ngoma alipouwahi kasha kumpiga chenga golikipa na kufunga goli
ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi
cha pili mpira kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi ya
kushtukiza na kurudi kulinda lango lao na katika dakika ya 72, Amissi
Tambwe aliiandikia Yanga goli la pili nala ushindi ambalo lilidumu hadi
mwamuzi, Jonesia Rukyaa anapiliza filimbi ya kumaliza mchezo huo.
Katika
mchezo huo timu zote zilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ili
kuona kama wanaweza kubadili hali ya mchezo ambapo kwa Simba walimtoa
Mwinyikazimoto, Hamisi Kiiza na Ibrahim Hijib na nafasi zao kuchukuliwa
na Nova Lufunga, Danny Lyanga na Brian Majwega.
Yanga
wao walifanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Niyonzima na Deus Kaseke na
nafasi kuchukuliwa na Simon Msuva na Godfrey Mwashiuya.
Vikosi:
Yanga: Barthez, Abdul, Bossou, Twite, Mgwali, Ngonyani, Kaseke, Kamusoko, Tambwe, Ngoma na Niyonzima.
Simba: Angban, Kessy, Tshabalala, Juuko, Banda, Majavi, Mkude, Kazimoto, Kiiza, Hijib na Ndemla.
EmoticonEmoticon