Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi
ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa
kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Malinzi
ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col.
Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka
kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu
Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na
kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika
hilo la B.
Washindi
wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda
Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo
miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.