WAZIRI wa maji
Mhandisi Gerson Lwenge pichani )kushoto ameombwa kuingilia kati na
kushughulikia kwa haraka utata
uliogubika utekelezaji wa mradi
wa Bwawa la maji
la malezi lilipo kata ya Malezi ,Mjini Handeni ambao
haujaanza licha ya Benk ya Dunia kutoa shs. 740 kwa
ajili ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na
wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo,
wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni
sababau ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa
alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya
ujenzi wa bwawa hilo ambao unatarajiwa
uwanufaishe Wakazi Zaidi ya 6000.
Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880.
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana
sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha
zilizoingizwa kaikamakauntinkuwa shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa nini
mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo
eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.
(Pichani kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini,Omari Kigoda)
Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya
Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi ammepokea wataalamu
ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya
kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizw kwenye mradi huo waache
kulima.
“Tunapata lawama kwa wananchi kwa
sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,”
alisema.
Naye Cecilia Ibrahimu wa
Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa
alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu wote.
“Sina cha kusema nataka maji tu. Cha
ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa
hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi. Cecilia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho
hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo
yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah
Kigoda.