Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limetuma salamu za rambirambi
kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo
cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani
Zanzibar.
Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu
jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu katika
kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili
(200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake
Suleiman Ally.
Mazishi ya marehmu Suleiman Ally Hemed mefanyika jana jioni mjini Zanzibar