WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS DOKTA MAGUFULI KUPAMBANA NA UFISADI-DR.WALUKANI

December 22, 2015
Mhitimu wa Shahada ya Udaktari na
Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi akizungumza wakati wa mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho


 DR.WALUKANI  LUHAMBA AKIPONGEZWA NA FAMILIA YAKE MARA BAADA YA KUHITIMU  SHAHADA YA UDAKTARI NA UZAMIVU WA FALSAFA KATIKA MASWALA YA UONGOZI KUTOKA CHUO CHA NEW LIFE BIBLE COLLEGE AND SEMINARY US CHENYE TAWI LAKE KATA YA MLANDIZI MKOANI PWANI KATIKATI NI MKEWE

WAHITIMU wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kumsaidia Rais John Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi uliokithiri kwa kuhakikisha hawajihusishi na masuala hayo katika maisha yao ikiwemo kutumia taalumu walizozipata kujipatia maendeleo wao na jamii zinazowazunguka.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mhitimu wa Shahada ya Udaktari na
Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi
mkoani hapa Walukani Luhamba mara baada ya kutunikiwa cheti cha kuhitimu kwenye mafalali iliyofanyika mjini hapa.
 

Alisema kuwa wahitimu hao wanaweza kutumia vizuri taaluma zao
walizozipata kuhakikisha wanazitumikia jamii zao ikiwemo kuwa wabuni katika kujipatia vipato halali ambavyo vinaweza kuwasaidia kwenye kukabiliana na maisha badala ya kusubiriwa kuajiriwa.

 

Dokta Luhamba  alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua wao wanafursa kubwa ya kuibadilisha jamii ili waweze kuondokana na masuala ya jamii tegemezi badala yake watumia nafasi walizonazo katika kujiletea maendeleo.
 

 “Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana ambazo zinaweza kutumika vizuri katika kuhakikisha wanajiletea maendeleo hivyo viongozi waliopewa dhamana na wananchi waangalie alama za nyakati na wafanya kazi kwa uadilifu mkubwa kama serikali ya sasa inavyofanya shughuli zake chini ya Rais Dr. Magufuli “Alisema Luhamba
 

Aidha aliwataka kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi zao kwa uadilifu na hekima kubwa ili kuchochea kazi ya ukuaji wa uchumi kwao na nchi kwa ujumla sambamba na kusaidia serikali kukabiliana na wabadhirifu wa mali za umma.
 

   “Lakini pia tuhakikisha tunakuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa na kumuombea Rais wetu Magufuli ili mungu aweze kumtia nguvu za kuweza kutekeleza kazi zake nzuri alizozianza kwa ueledi mkubwa na ufanisi katika kulipatia maendeleo Taifa letu “Alisema Walukani.
 

Katika mahafali hayo zadi ya  wahitimu 30 walitunukiwa vyeti na mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Proffesa John Adamson Mwakilema lakini kwa upande wa Shahada ya Udaktari na Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi walikuwa wahitimu wawili akiwemo Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) Mkoa,Dr.Walukani Luhamba.
 

Proffesa Mwakilima aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika jamii zao kwa kutumia vizuri taaluma walizozipata katika kuinua uchumi wao na wananchi wanaowazunguka.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »