Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari
ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa
hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani
ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John
Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala
chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan
Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman
Wanin Kiloloma.
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia),
Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati
baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa
anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba
mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji
wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika
Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya
ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine
amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema
amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na
kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa
kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja
wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri
wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za
serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali,
Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia
mifumo ya Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya
kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji
wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.
EmoticonEmoticon