
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawako pichani) leo tarehe 23/11/2015 katika Ofisi
za Wizara hiyo ambapo amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha
miaka minne. Uchaguzi huo umefuatia uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa nchi
Wanachama wa Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) unaohusu Urithi wa Dunia uliofanyika mjini Paris,
Ufaransa tarehe 18-20 Novemba 2015. (Habari Kamili SOMA TAARIFA KWA UMMA
HAPO CHINI)

Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru kushoto
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Tanzania kuchaguliwa
kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia. Alieleza kuwa katika Kamati
hiyo Tanzania itawakilishwa na Bw. Donatius Makamba ambaye ni
Mkurugugenzi Idara ya Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii
akisaidiwa na Dkt. James Wakibara, Mwikolojia Mkuu wa Shirika la Hifadhi
ya Taifa (TANAPA) na Dkt. Mohammed Juma, Mkurugenzi wa Mipango Miji na
Vijiji kutoka Zanzibar.

Bi.
Eliwasa Maro Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Mafunzo na Takwimu Wizara ya
Maliasili na Utalii akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika Mkutano
huo na Waandishi wa Habari.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakinukuu baadhi ya mambo muhimu.


EmoticonEmoticon