Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower
akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao sambamba na Sony Masamba jumapili
iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza kiota cha Escape One
Mikocheni jijini Dar es Salaam na hivi leo mwendo ni ule ule na speed
120.(Picha na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Rapa Joniko Flower akichuana na mmoja wa shabiki wa Skylight Band
staili mbalimbali za sebene huku mashabiki wengine wakiangalia na kuiga
miondoko hiyo.
Msanii
Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje akijumuika kuwapa raha mashabiki
wa Skylight Band jumapili iliyopita kwenye kiota cha Escape One,
Mikocheni jijini Dar…Kwa mbali ni Tophy Bass akicharaza nyuzi kisawa
sawa.
Msanii
Em Evans kutoka bendi ya Wana Njenje sambamba na Kasongo Junior wa
Skylight Band katika kolabo matata sana kuonyesha kipaji chao, njoo leo
uwashuhudie Live kiota cha Escape One Mikocheni.
Em Evans na Kasongo Junior wakiendelea kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi kutoka Skylight Band, Joniko Flower
katika hisia kali kuwapa raha mashabiki wake kiota cha Escape One,
Mikocheni jumapili iliyopita ambapo leo pia mwendo ni ule ule, bila
kukosa njoo wewe na yule waambie na wengine pia bila kukosa katika fukwe
tulivu kabisa.
Kasongo Junior katika hisia kali sambamba na Joniko Flower kwenye kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo
pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa
ya leo itakuwa pale pale.
Bamutu wa Congo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band Joniko Flower
na Sony Masamba ni ndani ya kioata cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Sam Mapenzi akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Sony Masamba na
Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili
iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani
iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight
Band.
EmoticonEmoticon