POLISI TANGA YAWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 45

November 08, 2015


Tangakumekuc
Tanga,POLISI Mkoani Tanga, imewakamata wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa katika gari aina ya fuso baada ya  kuwepo kwa taarifa ya  watu hao kusafirishwa kutoka Moshi Mkoani Kilimanjaro kueleka Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6 usiku katika kizuizi cha polisi cha Mombo Wilayani Korogwe.
Alisema watuhumiwa hao waligundulika wakiwa wamefichwa katika gari aina ya fuso ambalo mlangoni na pembezoni mwa gari iliwekwa  mikungu ya ndizi ili kuwaficha lakini polisi ilitilia shaka baada ya kusikia minong’ono ya sauti za watu ikitokea ndani ya gari.
Kamanda Mombeji aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Mlacho Mathias (24) Oleso Bafe (22) Dameke Lodore (20) Damekglo Achore (20), Jose Yosete (25), Tarafa Kajamo (18), Aserat Eleysa (17), Dagu Sumoro (40), Akililu Abeba (22), Aberhame  Tadewose (20), Abara Adese (30) , Ayrno Bekele (20),  Taseme Workicho (20), Adam Ashore (21), Tamasegen Tumoro (19), Baharu Detamo (21), Sekadu Ababea (23), Wondem Wakere (24), Tamerat Dafar (21), Beruke Kelebore (21), Nuruden Tamso (22), Dekebe Abebe (17), Mulegeta Alam (20), Chakebo Muhaba (22), Alamayu Tasama (23), Manegestu Marko  (24), Kayadayn Nourgaba (24), Eleyas Eregano (24), Tasama Herama (18), Adese Kate (22), Daraje Damaka (22), Ramato Atoro (23), Damake Damerati (25), Workicho Kidir (20), Tamasgen Lamango (20), Sambatno Asafa (23), Takatare Tsagaye  (22), Takala Aniko (17), Kabada Tadewose (16), Mide Mhamade (25) Dandem Deledele (23), Dagenet Wolede (25) , Gelachu  Tadese (20), Lere Abdella (18)  na Thomas Kibamo (21).
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa kituo kikuu cha Polsi cha Chumbageni na wanahojiwa na mara baada kukamilika upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kuingia nchini bila kibali.
Alisema mbali ya wahamiaji hao pia inawashikilia Watanzania watano kwa tuhuma za kuwasafirisha Waethopia hao akiwemo dereva wa Fuso Khamis Ally (31) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam pamoja na utingo na watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ally Haruni (17) ambaye ni utingo mkazi wa Tegeta, Mussa Shaban (30) fundi gari mkazi wa Kinondoni MkwajuniYohana Teherera (22) mfanyabiashara wa Dar es Salaam na Fadhilui Hussein  (27) fundi muashi na mkazi wa Muheza Tanga.
“Wale wahamiaji walikuwa wamewekwa katika fuso huku mlangoni walikuwa wameweka mikungu ya ndizi pamoja na pembezoni kwa ubavu wa gari ili kuwalaghai polisi njiani ambapo njama zao ziligonga mwamba” alisema Mombeji na kuongeza
“Wakati gari iliposimamishwa na askari wanalikagua walipoulizwa wakadai kuwa wamepakiza ndizi na kupeleka Dar es Salaam---mara wakasikia watu wanakohowa na minong’onomong’ono na kugundua rundo la watu ndani” alisema
Kamanda alisema watu wote wanashikiliwa na polisi kituo kikuu cha Chumbageni pamoja na gari kwa mahojiano na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kusafirisha wahamiaji haramu.





 Wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa katika uwanja wa ndani ofisi za Uhamiaji Tanga jana waliokamatwa Mombo Wilayani Korogwe waliokuwa wakisafirishwa kuelekea Dar es Salaam kwa kutumia gari aina ya Fuso.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »