WAISLAMU WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWASAIDIA WENZAO WASIO NA UWEZO

September 24, 2015


Waumini wa dini ya Kislaamu Mkoani Tanga wakiwa kwenye ghafla ya kuchinja ng’ombe  hamsini waliotolewa na wahisani REFSO  kutoka nchini Uturuki  kwa ajili ya siku kuu hiyo





Waislamu nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuwasaidia waumini wasio jiweza katika kutekeleza ibada tukufu ya Eid –el  Haj,inayoambatana na kuchinja ili wote wawe miongoni mwa waliopata razi za Mwenyezi Mungu.
Wito huo ulitolewa jana kwenye ghafla ya kuchinja ng’ombe  hamsini waliotolewa na wahisani REFSO  kutoka nchini Uturuki  kwa ajili ya siku kuu hiyo na Mwenyekiti wa Umoja wa Wasomi wa Kiislamu Mkoa Tanga(Tampro), Nyumbwe Mwariko ambapo alisema jambo hilo ni kheri kwa umma wa kiislam na wameipokea kama changamoto.
Mwariko akiwa katika shughuli hiyo katika  viwanja Neema Jijini Tanga alisema kuwa tangu mwaka 2010 wahisan hao kutoka Uturuki wamekuwa mstari wa mbele kuwajali waislam wasiojiweza hapa nchini na kushirikiana nao katika ibada hiyo na kutoa idadi kubwa ya ng’ombe kwa mikoa kumi nchi nzima .
Aidha alisema ndani ya nchi yetu hususan mkoa wwetu wa Tanga wapo watu waliokuwa na uwezo mkubwa lakini kwa kutokuthamini umoja,mapenzi ,mshikamano kwa umma wa kiislam kumepelekea kujenga matabaka.
 “Niseme hakuna waislam Mwenyezi Mungu aliowaruzuku, ni kutokuwa na imani ndani ya mioyo yao na kusababisha kutowajali wale wasiojaaliwa” alisema Mwariko.
Hata hivyo alisema chama hicho  kwa kushirikiana na REFSO ya nchini Uturuki wamejipanga kutekeleza ibada hiyo kila mwaka kwa ufanisi zaidi ili kuwasaidia waislam wote wasiojiweza mkoa mzima wa Tanga kwa siku hiyo adhwimu ya Eid El haji.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »