Mh Davis Mosha akiwa na Mwenyekiti wa KDFAA Ndugu Msasu.
Mgombea Ubunge wa Moshi
Mjini kupitia Tiketi ya ccm Mh. Davis Mosha Amekutana na wasanii wa
Filamu, Maigizo ya Jukwaani, Sarakasi na Muziki wa Mjini moshi. Wasanii
hao wakiongozwa na Chama cha Wigizaji na wacheza filam Kilimanjaro
(KDFAA)
Wasanii hao walioomba
Mkutano na Mh. Davis Mosha leo katika ukumbi wa ccm Mkoa walipata fursa
ya kuzungumza Changamoto zinazowakabili na Malengo yao kama wasanii wa
Moshi na Mkoa Kilimanjaro. Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ukumbu
huo mmoja wa Wasanii wa Muziki Ndugu Samwel Stephen aliweza kumuomba Mh.
Davis Mosha awasaidie kupata studio ya kisasa na kuwapa wigo mpana wa
kazi zao za muziki kuweza kupigwa katika Radio.
Mh. Davis Mosha akijibu
hilo aliwahakikishia Kujenga Studio ya Kisasa itakayoanza kufanya kazi
mapema Mwezi ujao chini ya Kampuni yake ya African Swahili Media
sambamba na Kufungua kituo cha Redio na Tv.
Wasanii wa Filamu
waliomba kuweza kusaidiwa kurekodi Tamthilia ambayo itaweza kurushwa
katika Tv na waweze kujitangaza na kujiajiri kupitia sanaa hiyo lakini
pia hawakusita kutoa kilio chao juu ya Wizi wa kazi zao unaofanywa na
wasambazaji pamoja na Wasambazaji kutoka Dar es Salaam kuwanyonya na
kusababisha kazi zao za Film kubaki nyumbani badala ya kwenda Sokoni.
Pia waliweza kutoa malalamiko yao juu ya uongozi uliokuwepo madarakani
katika ngazi ya ubunge na Udiwani kuwaahidi maramara ahadi ambazo
hazitekelezeki.
Mh Davis Mosha akifafanua Jambo katika Mkutano na Wasanii Leo
Bwana Mosha aliweza
kuwahakikishia Soko la uhakika la filam zao na pia ulinzi wa kazi zao
kupitia vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya haki miliki na pia
kuweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao. Na pia aligusia suala la
wasanii wa Ngoma za asili juu ya kuhakikisha anaweka kituo cha sanaa na
utalii ili kuweza kuwakutanisha wageni wanaokuja kupanda mlima na
kufanya ni kituo cha kubuudika kupitia ngoma za asili na sehemu ya
kujifunzi aTamaduni za Makabila mbalimbali ya Tanzania. LAkini pia
aliwaasa wasanii kutumia sanaa yao kutoa elimu ya uchaguzi juu ya
wananchi kutumia haki yao ya msingi katika kuchagua na wasifanye makosa
watumie Mitaji yao ya Vitambulisho vya kupigia kura kuhakikisha
wanachagua Kiongozi atakayeenda kufanya kazi na si mwanasiasa.
Mwenyekiti wa KDFAA akitoa shukrani zake kw Mh. Davis Mosha kwa Kukubali kuja kuwasikiliza.
Akifunga Mkutano huo wa
wasanii, Mwenyekiti wa Chama cha waigizaji na Filamu Ndugu Msasu alitoa
shukrani za Dhati kwa Mh. Davis Mosha huku akimfananisha na Mkombozi
ambaye amekuja kuwakomboa kutokana na Viongozi wengi kuwadharau wasaniii
na kupelekea Sanaa ya Moshi kuzidi kushuka. Alitumia nafasi hiyo
kuwaasa wasanii kutochezea nafasi waliyopata ambayo Mh. Davis Mosha
ameonesha nia ya dhati ya kuweza kuwakomboa kupitia sanaa yao na wao
basi waoneshe hitaji lao kwake kwa kuhakikisha wanafanya kazi nzuri
katika sanaa
EmoticonEmoticon