Wizara
ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma kuwa, Bodi mpya ya
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife
Authority -TAWA), imeteuliwa rasmi kuanzia tarehe 09 mwezi Septemba,
2015.
Katika uteuzi huo, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Rajabu SEMFUKO kuwa Mwenyekiti
wa Bodi hiyo.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo
ambao wameteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ni Dkt. Simon Mduma –
Mkurugenzi Mkuu – TAWIRI, Dkt. Fred Manongi – Mhifadhi Mkuu – NCAA,
Suzane Charles Ndomba – Mwanasheria – ATE, Bw. Gerald Bigurube –
Meneja wa Program Frankfurt Zoological Society – SERENGETI, Dkt. David
Manyanza (Mstaafu) Mtaalam wa Maswala ya Wanyamapori , Bw. Benson A.
Shallanda – Kamishna wa Sera – HAZINA, Jenerali Samweli Ndomba –
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Winfrida Nshangeki – Mkurugenzi wa
Uratibu wa Sera – TAMISEMI, Abdulrahman Kaniki – Naibu Mkuu wa Jeshi la
Polisi Tanzania , Allan J. Kijazi – Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mr. Herman
W. Keraryo –Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Abdul Rajab
Mhinte – Mkuu wa Idara ya Usalama na Atakayeteuliwa kuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka .
Bodi hii, itaongoza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.
Imetolewa na
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Maliasili na Utalii
21/09/2015
EmoticonEmoticon