KERRY AMFICHA MSENEGAL

September 12, 2015
KOCHA Mkuu wa Simba, Kerry Dylan ameonekana kuficha ukweli juu ya hatma ya Mshambuliaji wa Kimataifa raia wa Senegal Pape N’daw kucheza mechi ya leo ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya African Sports kwa kusema itategemea na kikoa cha awali kabla ya mechi hiyo.
 
Akizungumza jana mara baada ya kumalizika  mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwa saa moja na nusu yakianzia saa mbili kamili na kumaliza saa tatu na nusu kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.

Kerry alisema kuwa mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota ambao wametua na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo huo.
 
Awali Kerr aliomba muda wa wiki mbili ili straika huyo awe fiti
vilivyo kucheza mecha za Ligi lakini kutokana na kukosa huduma na nyota wake Ibrahim Ajibu huenda akamtumia N’daw kama chaguo la pili katika kikosi chake hii leo.

Alisema licha ya kukosekana Ajibu kwenye mechi hiyo lakini wachezaji kadhaa nao wanaweza wasionekana kama vile Abdi Banda,Jonas Mkude,Mohamed Fakhi ambao watashindwa kuonekana kutokana na kuwa na majeruhi.

Aidha inaonekana kuwa kuna hatihati ya beki wa kati,Isihaka Hassani akashindwa kuonekana kwenye mchezo huo kutokana na jana kushindwa kuungana na wenzake kwenye mazoezi kwa kufanya yale mepesi ili kuweza kujiweka imara kuelekea mchezo huo.
 
Hali kadhalika kuelekea mechi hiyo,shamra shamra za kuelekea mechi hiyo zimeonekana kupamba moto kutokana na kila kona ya mji huu kuonekana kutawala tisheti nyekundu ambazo zimekuwa zikiuzwa tokea juzi asubuhi hali inayoonyesha hari ya mechi hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »