WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIIANA NA SHIRIKA LA HELPAGE INTERNATIONAL WAMEANDAA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KUTATHMINI HUDUMA BORA ZA WAZEE ZANZIBAR KATIKA HOTELI YA OCEAN VIEW.

September 12, 2015

 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar ulioandaliwa na Wizara yake kwa ufadhili wa Shirika la HelpAge International katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Naibu Mkurugenzi wa Shirika la HelpAge Internalinal  Smart Daniel akizungumza na washiriki wa Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View Kilmani (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na kushoto Mwenyekiti wa Mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Haji Makungu Mgongo. PICHA NA RAMADHANI ALI / MAELEZO ZANZIBAR.
 Washiriki wa Mkutano  huo wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana juu ya mikakati itakayofanikisha kuandaliwa mazingira bora ya maisha ya Wazee Zanzibar.
 Daktari Dhamana  Wilaya ya Wete akiwasilisha kazi za vikundi katika mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Saleh Muhammed Jidawi akifunga mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Zanzibar, Madaktari dhamana wa Hospitali kuu za Wilaya, Jumuia ya Wazee  na Taasisi za kiraia baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »