Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Mkurugenzi
wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa wakati alipowasili kwenye
klabu ya Yacht ya Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji
watanzania kutembelea Mbuga za Taifa iliyozinduliwa leo jijini Mwanza
ikiwashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Katika Picha kulia ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan
Kijazi.
Kampeni hiyo ambayo inaanza kesho Julai 1 itakuwa ni ya miezi 6
mpaka Desema 31 na kauli mbiu yake inasema “Tembelea Hifadhi
Uzawadiwe”.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi
akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi.
Devotha Mdachi wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi
akifuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wakati
alipowasili kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji Watanzania
kutembelea Mbuga za taifa kulia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA
Bw. Ibrahim Mussa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiongozana na Mkurugenzi wa
Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa na Johnson Manase Meneja wa
Utalii TANAPA.
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
Baadhi ya maofisa wa TANAPA wakiwa katika uzinduzi huo
Wahariri wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo
Mwandishi Jimmy Mengere na Kasilda Mrimira wakiperuzi simu zao wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii akiwa katika meza kuu wakati hotuba za viongozi
mbalimbali zikiendelea kulia ni Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi na
kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi
wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa na Katibu Tawala wa mkoa wa
Mwaza Bw. Faiza Issa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa akizungumzia kampeni hiyo.
Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza leo.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa kulia na Kaimu Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi. Devotha Mdachi wakifuatilia matukio
katika hafla hiyo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Faiza Issa akimkaribisha Waziri wa
Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu ili kuzungumza katika uzinduzi
huo.
Baadhi ya magari ya kubeba watalii yaliyozinduliwa leo katika kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Mwanza.
Waziri Nyalandu akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
Waziri
Nyalandu akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo na
kuwaasa wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki kikamilifu katika Kampeni hiyo
Waziri
Nyalandu akikata utepe kuzinduz boti maalum za kubeba watalii kutoka
jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Saanane kwa ajili ya kujionea utalii
ulioko katika kisiwa hicho.
Waziri
Nyalandu akiwaaga baadhi ya watalii wa ndani waliokuwa wakiondoka na
boti kuelekea kiswa cha Sanane kilichopo mkoani Mwanza.
Boti iliyobeba watalii hao wa ndani ikiondoka jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Sanane
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa magari ya kubeba watalii jijini Mwanza katika mpango
wa kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea mbuga za taifa.
Waziri
Nyalandu akipiga picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mara
baada ya kuzindua magari ya kubebea watalii jijini Mwanza.
Waziri Nyalandu akiwaaga watalii hao wakati walipokuwa wakiondoka.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi na
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wakipiga picha ya
pamoja na kupongezana mara baada ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akiwaaga watalii hao wakati walipokuwa waiondoka.
EmoticonEmoticon