BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED'

May 24, 2015

 Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae ,Lets Get Married iliyichezwa na wachina na kutafsiriwa kwa kiswahili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar e Salaam jana. Kulia ni Ofisa kutoka ubalozi wa China, ambaye alikuwa ni mkalimani wa balozi huyo, Yetianfa Attache.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

 Maofisa wa Kampuni ya StarTimes wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Warembo wa StarTimes wakiwa tayari kwa zoezi la kuzindua Tamthilia hiyo. Kutoka kulia ni Hadija Saidi, Nyachilo Bunini na Fausta Mushi.
 Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta'  (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale


BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.


Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane 'Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.


"China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta  ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa" alisema Balozi Dong.


Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.


Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.


Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »