Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja wa Mataifa wiki hii, umekamilisha mikutano muhimu miwili kati ya mingi, ambapo ujumbe wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ulioshiriki majadiliano
ya mikutano hiyo waliiwakilisha vema nchi yao.
Moja ya mikutano hiyo
ni ule wa marejeo
ya Mkataba wa kuzuia usambaaji na uzalishaji wa silaha
za nyukilia, matumizi yake, ikiwa ni pamoja na silaha nyingine za maangamizi (
NPT), Mkutano huu ambao umefanyika kwa
mwezi mzima, ukitawaliwa na majadiliano makali juu ya mada
mbalimbali muhimu zinazohusiana na
marejeo ya mkataba huo. Bado hadi
siku ya mwisho ya mkutano ( Ijumaa)
wajumbe wamemaliza mkutano pasi kufikia makubaliano ya pamoja ya vipengele kadhaa vya tamko la
mwisho la mkutano.
Katika kile kilichooneka wazi kwamba wajumbe wamekubali kuto kukubaliana, ni kwa baadhi ya
mataifa hasa yale ya magharibi na
yenye silaha za nyukilia kutoonyesha utayari na utashi wa kisiasa wa kuungano
mkono baadhi ya mambo kadhaa
likiwamo la kufanyika kwa mkutano wa
Ukanda Huru usio na silaha za Nyukilia katika Eneo la Mashariki
ya Kati .
Mataifa kama vile Marekani, Uingereza na Canada yalisimamia kidete
misimamo yao ya kupinga kuingizwa katika
tamko la mwisho la mkutano wa NPT
sehemu inayopendekezwa kufanyika kwa mkutano huo huko Mashariki ya Kati, kwa kile walichodai kwamba
baadhi ya mataifa yamelipenyeza suala
hilo bila ya ushirikishwaji wa nchi nyingine ikiwa Israel jambo ambalo wamesema
hawakubaliani nalo.
Mkutano kuhusu ukanda huru usio wa silaha za nyukilia
katika eneo la Mashariki ya Kati, umeshindikana kufanyia kwa muda mrefu sasa
licha ya maazimio mbalimbali
yanatoaka ufanyika.
Kushindwa kwa mkutano huo ambao unaelekezwa kama muhimu kwa
mustakabali wa hali ya amani na
usalama katika eneohilo, unatokana kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa
uungwaji mmono usio na shaka kutoka kwa
wadau mbalimbali ikiwamo Israeli ambayo imekuwa ikilalamikwa na baadhi ya
mataifa ya Kiaarabu.
Israel
si mwanchama wa NPT. lakini pia inasadikiwa inamiliki silaha za
nyukilia ingawa haijatamka hadharani. Mataifa mengi yakiwamo
yakiiarabu yamekuwa
yakilitaka taifa hilo kutamka mbele
ya Jumuiya ya Kimataifa kwamba
inamiliki silaha hizo lakini imekuwa
ikikingiwa kifua na baadhi ya mataifa
makubwa.
Eneo jingine ambalo
wajumbe wameshindwa kukubaliana kwa kauli moja ni pendekezo la
kuingizia kwenye mkataba huo sehemu
itakayozungumzia madhara ya kibinadamu
yatakayo na matumizi ya silaha za
nyukilia. Eneo hili nalo limezua mjadala mzito kiasi kwamba licha
ya umuhimu wake kwa uhai wa mwanadamua na viumbe hai
likashindwa pia kufikia makubaliano ya pamoja.
Rasmu ya
tamko la mwisho la mkutano huo
limepitishwa kwa vifungu kutokana
na kile ambacho wajumbe wamesema ni kutoridhishwa kwa maudhui mazima ya tamko hilo huku wengine wakieleza kwamba,
baadhi ya vifungu ambayo vilipitishwa kwa
makubaliano wakati wa majadiliano ya wiki nne havikuingizwa katika tamko hilo
Wazungumzaji wengi katika siku ya mwisho ya mkutano huu ambao
ulikwenda hadi saa tatu usiku, siku
ya ijumaa, wameelezea masikitiko
yao ya kukosekana kwa fursa ya kusukuma mbele utekelezaji wa NPT kwa sababu tu ya baadhi ya nchi kusimamia
maslahi binafsi badala ya maslahi ya jumla.
Mkutano wa pili
ambao nao ulikuwa na mvutano wa aina yake ni ule uliokuwa ukijadili maandalizi ya
ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs).
Mkutano huu wa wiki moja na ambao pia
ulimalizika siku ya ijumaa, wajumbe
licha ya kukubaliana na maudhui mazima
ya haja na umuhimu wa kufanyika kwa tathmini na ufuatiliaji wa
utekelezaji wa SDGs, wajumbe walishindwa kukubaliana kwa kauli
moja mada au ajenda zitakazo jadiliwa
wakati wa mkutano wa Kisiasa wa Ngazi ya
Juu wa viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika mwezi Septemba 2015
Mkutano huo wa Kilele wa Kisiasa wa viongozi unatarajiwa
kupokea na kupitisha ajenda na malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015, mkutano ambao pia utakuwa na miduara ya
majadiliano ya maada mbalimbali.
Katika maandalizi ya mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliziomba nchi
wanachama kuunda mada zikazojadiliwa katika mkutano huo,
maanda mabazo kimaudhui zinatakiwa kwenda na
SDGs.
Kwa wiki kadhaa
nchi wanachama kupitia makundi
yao ya kikanda walikuwa na kazi kubwa ya
kubuni mada hizo, kuzijadilia na kisha
kukubaliana zile ambazo wanaamini ndizo
muhimu.
Mada ambazo zimependekezwa ni
pamoja na mada itakayojadili kumaliza umaskini na tatizo la njaa,
kukabiliana na ukosefu wa usawa, uwezeshwaji wa wanawake na wasichana bila
kuacha mtu nyuma, kukuza uchumi endelevu na kuleta mabadiliko katika uzalishaji na kiwango cha matumizi na kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi ili kuilinda
dunia.
Mada nyingine zinazopendekezwa ni kujenga ufanisi, uwajibikaji ili kufikia
maendeleo endelevu, kukuza ushirikiano wa kimataifa, kujenga misingi imara ya
uwajibikaji na taasisi jumuishi ili kufikia maendeleo endelevu na kukuza ushirikiano wa kimataifa.
Pamoja
na kukuballiana juu ya mada hizo, washiriki wa mkutano huu
walishindwa kukubaliana juu ya maudhui
pana iliyoainisha kila mada. Kutokana nakwamba kila nchi au kundi
wakilishi lilikuwa na tafsiri tofauti ya maelezo ya ziada ya
mada hizo.
Matokeo
ya kushindwa kukubaliana kuhusu maudhui pana au maelezo yakina ya
baadhi mada na baada ya majadiliano ya
kujaribu kupata muafaka kati ya pande zinazopinga kushindwa
kuafikiana, Wenyeviti- wenza wa majadiliano hayo walieleza kwamba
kutokana na wajumbe kutokubaliana basi mada hizo zitapelekwa kwa Rais
wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
kwa maamuzi.
EmoticonEmoticon