WAGONJWA wapatao 3000 kutoka maeneo
mbalimbali mkoani Tanga wenye matatizo ya macho wameanza kunufaika na huduma za
kufanyiwa uchunguzi wa pamoja na matibabu
kwenye Hospital ya Shifaa Charitable Health Centre iliyopo mjini hapa.
Matibabu hayo yaliyoanza kutolewa
Mei 16 mwaka huu ambayo yalimalizika jana yakiwa na
lengo la kuwafanyia upasuaji wa aina mbili wananchi wenye matatizo ya macho ili
kuweza kubaini matatizo wanayokabiliana nayo na kuyapatia huduma.
Akizungumza jana, Naibu Mudir wa
Taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center,Sheikh Salim Bafadhil alisema kuwa
upasuaji huo unalenga kwenye mambo makuu mawili yakiwemo ya kuondoa mtoto wa jicho
na utandu uliopo ndani ya macho ambayo inaendesha na hospitali hiyo chini ya
udhamini wa Al Basar International Foundition kutoka Saudi Arabia.
Alisema kuwa zoezi hilo linaendeshwa
na madaktari kumi na mbili waliotoka nchini Pakistani wakiongozwa na daktari
Fakhruddin Dakhan ambapo kwa siku wanahudumia wagonjwa wa macho wapatao 300
ambayo wanakwenda kwao kwa ajili ya matibabu.
“Mpaka jana(juzi) tumeweza kufanya upasuaji zaidi ya wagonjwa 130 na
kubwa ni kuangalia matatizo makubwa kwenye macho kama vile kuondoa motto kwenye
jicho na kuondoa utandu kwenye macho kwa
kushirikiana na madaktari hao “Alisema Naibu Mudir huyo.
Aidha alisema kuwa lengo kubwa lao
ni kuhakikisha wanatoa huduma kwa jamii ya wananchi wenye matatizo hayo ili
waweze kupata nafuu na kuweza kufanya kazi mbalimbali za kijiingizia vipato
kama ilivyokuwa kawaida yao kabla ya kukumbana na changamoto hizo.
EmoticonEmoticon