AMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI
Kocha Jackson Mayanja wa Kagera
Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa
lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa
Sugar kuwa walipewa rushwa.
Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja
kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya
Ligi Kuu.
Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa
faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati
wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa
Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Adhabu hiyo
imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.
Nayo Simba imepigwa faini ya sh.
300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao
kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera
Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.
Pia Simba imepigwa faini ya sh.
500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile
kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba
146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.
Kipa Tony Kavishe wa Polisi
Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa
la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa
kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi
namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
KAMATI YA MASHINDANO TFF
Kamati ya Mashindano ya TFF
ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi
karibuni.
Katika matukio ya SDL, Kamati
imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa
kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo
kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri
Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi
Daraja la Pili.
Nao makocha wa JKT Rwamkoma,
Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja
na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja
katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.
Wachezaji Shafii Maganga, Saleh
Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa
kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye
Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.
VPL KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini,
jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya
Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Mjini Morogoro wakata miwa wa
Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini
timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba
la Manungu Turiani.
TTF YAFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI VIJANA
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa
Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa
miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.
Akiongea na waandishi wa habari,
Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka
mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa
baadae.
Vijana hawa mnaowaona hapa
wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na
kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu
watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya
kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania
inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.
Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi
ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya
Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi
waje kuwa waamuzi wa kimataifa.
Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa
kufungwa ijumaa tarehe 17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya
Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana
37 waamuzi wawili ni wanawake.
Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.
EmoticonEmoticon