Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu baadhi ya Shule za
Sekondari za Bweni zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula ambapo
alisema shule hizo zimefungwa kimakosa kwani Serikali imeshapeleka fedha
za kununulia chakula kwenye halmashauri zote nchini. Kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba.
Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI
Bw. Zuberi Samataba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam mpango wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za
msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada badala ya Cheti kama ilivyo sasa.
Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne
Sagini wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye ofisi za TAMISEMI jijini
Dar es Salaam.
Picha na Fatma Salum (MAELEZO)
EmoticonEmoticon