Edward Lowassa aungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka

April 04, 2015

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa ameungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front la Dar es Salaam leo.
Ibada ikiendelea.
Sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika leo.
 
Igizo la Yesu likiongozwa na Bw. Moses Kombe alivyokuwa na wanafunzi wake kabla ya kuteswa hadi kutungikwa msalabani, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam leo.
Mh. Edward Lowassa akifatilia igizo la mateso ya Yesu, lililoigizwa na Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Igizo likiendelea.
Mmoja wa watoto waliokuwepo Kanisani hapo akiangalia Igizo hilo.
Mmoja wa Waigizaji hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipitia vifungu vya Biblia wakati Igizo la Yesu likiendelea.
Yesu akipelekwa kwa Pilato.
Vijana hao wakiigiza pale Yesu alipofikiswa kwa Pilato kuhukumiwa, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front Dar es Salaam
Huzuni ilitawala wakati wa Igizo hilo.
Yesu akiwa amebebeshwa Msalaba katika Igizo hilo.
Muumini wa Kikristo, Moses Kombe akitungikwa msalabani kama Yesu katika igizo lililofanywa na Vijana wa Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Kuna waliomlilia na Wengine kufurahia.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »