KINANA AMALIZA ZIARA YAKE SAME MAGHARIBI, KESHO KUENDELEA SAME MASHARIKI

March 27, 2015

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya Njoro wilayani Same, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SAME) 2 
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mh. David Mathayo David akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Njoro wilayani Same.
3 
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu huku wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipowasili katika kijiji cha Suji. 7 
Wana CCM wakiimba nyinbo za kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huo mjini Same.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »