Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua
kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na
teknolojia.
Aliongea
hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia
marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu
ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
“ubunifu
katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa
vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna
umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo
mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.
Aidha
aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika
sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta
maendeleo kwa jamii zao.
Vilevile
alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta
mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na
miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.
“Mfano
mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa
wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na
teknolojia ” alisema Balozi Sefue.
Aidha
aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali
kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana
kuvumbua teknolojia mbalimbali.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa
warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na
Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika
Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika)
akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John
Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya
Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia John Mngodo
akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa
sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, kushoto ni Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia
Prof. Evelyn Mbede .
Mkurugenzi
wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede, akiwasalimia wajumbe wa
warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na
ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na
Teknolojia Prof. Patrick Makungu, Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue na wa mwisho kulia ni Naibu katibu Mkuu waWizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngodo .
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick
Makungu, akisema hotuba ya kumakribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue(Hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya
ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia iliandaliwa na
Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Wadau
mbalimbali ambao ni wajumbe wa mkutano wa ubunifu wa sera ya taifa ya
Sayansi na teknolojia ilifanyika katika hoteli ya Kunduchi jijini Dar es
Salaam iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na
Teknolojia.(Picha na Lorietha Laurence- Maelezo)