Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi Mjini
Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa
Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi
tarehe 15.3.2015 kuanza ziara ya kikazi ya siku 5 kukagua utekelezaji wa
Ilani ya CCM.
Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha
Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya
wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Kata ya Mikumbi tarehe 16.3.2015.
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM Ndugu Shaibu Rajabu
Matola mara baada ya kujiunga na chama hicho. Ndugu Matola ni miongoni
mwa vijana 200 waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi
katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa
Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia ya wana CCM
na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata
ya Mikumbi katika Manispaa ya Lindi tarehe 16.3.2015.
Taswira mbalimbali za mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Kata ya Mikumbi, Manispaa ya Lindi na
kuhutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete tarehe 16.3.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
Mama Salma Kikwete akikabidhi bati 100 na vifaa vya bendi kwa uongozi
wa Shule ya Sekondari Angaza iliyoko katika Manispaa ya Lindi tarehe
16.3.2015. Anayepokea kwa niaba ya shule hiyo ni Mkuu wa Shule Mwalimu
Upendo Muro (wa tano kutoka kulia) akiwa pamoja na Ndugu Ashimun Mzava,
Afisa Elimu Sekondar, Manispaa Lindi wa nne kutoka kulia) na baadhi ya
wanafunzi wa shule hiyo. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Kilwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bwana Abdallah Ulega.