CHRISTIAN BELLA KUTUMBUIZA USIKU WA NANI KAMA MAMA KESHO HARBOURS CLUB

March 13, 2015
MSANII mahiri wa Mziki wa Dansi hapa nchini kutoka kundi la Malaika Band, Christian Bella (kulia)anatarajiwa kutumbiza katika onyesho la Usiku wa Nani Kama Mama litakalofanyika Machi 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Harbours Club jijini Tanga.

Akizungumza LEO,Mratibu wa Onyesho hilo,Mbwana Imamu ambaye ni Mkurugenzi wa Arbab Intertainment alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika kwa asilimia kubwa ambapo msanii huyo atatua mkoani hapa siku moja kabla.

Alisema kuwa onyesho hilo litakuwa ni maalumu kuwapa raha wakazi wa jiji la Tanga ambao walikuwa wameikosa kutoka kwa msaani huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa “Nani Kama Mama” na nyengine nyingi.

  “Unajua wakazi wa jiji la Tanga ni watu wa burudani hivyo uwepo wa Bella kwenye onyesho hili utawapa ladha mashabiki wake kutokana maeneo mbalimbali hivyo hawapaswi kuikosa badala yake wajitokeze kwa wingi “Alisema Mbwana.

Aidha mratibu huyo alisema kuwa baada ya kumalizika onyesho hilo wapenzi na mashabiki ambao watakuwa wamejitokeza watahamishia shangwe kwenye ukumbi wa Club Lacasachika.

  “Hii itakuwa ni baada ya kumalizika kwa party …. Wapenzi wa mziki huo watatumia nafasi hiyo kubadilishana mawazo na kutafakari namna onyesho hilo lilivyokwenda kwa kuendelea kupata burudani kwenye Club hiyo “Alisema Mratibu huyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »