Airtel yaitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Arusha

February 08, 2015

Meneja Mauzo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha , wakishuhudia (katika) Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma.
Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala (kulia) ,Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha.
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika) akiongea na wandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha wakishuhudia Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mkoani Arusha wakifatilia kwa makini uzinduzi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi uliofanyiaka katika hotel ya Palace Arusha leo ijumaa.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetambulisha promosheni yake ya Airtel yatosha kwa wakazi wa Arusha  na kusisitiza kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku.
Akiongea na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Amesema “tumeona ni vyema kutambulisha  promosheni hii kwa wakazi wa Arusha kwani wao pamoja na watanzania katika mikoa mbalimbali  wananafasi ya kujishindia. Promosheni hii tuliyoizundua rasmi mwanzoni mwa wiki hii inampa nafasi mteja wa Airtel kushiriki na kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST pindi atakaponunua kifurushi chake chochote cha Airtel yatosha”
Matinde aliongeza kwa kusema ”Mteja atakaponunua kifurushi chake cha siku anaingia kwenye promosheni kwa simu hiyo lakini akinununa cha wiki namba yake itaingia kwenye promosheni kwa muda wa siku saba na akinunua cha mwezi namba yake itaingia kwenye droo kila siku kwa siku thelathini.  Lakini mteja atakaponunua kifurushi chake cha Airtel yatosha cha siku zaidi ya mara moja namba yake itaingia kwenye droo ya siku hiyo kwa idadi ya vifurushi vya siku alivyonunua.
Ili kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha Mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kununua vocha ya yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money
Huduma ya Airtel yatosha inampa fulsa mtumiaji wa huduma yetu ya Airtel yatosha kupata vifurushi bora na vya bei nafuu sokoni lakini pia inamuwezesha kushinda Toyota IST aliongeza Matinde
Kwa upande wake Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini Bwana Brighton Majwala alisema, “promosheni hii ni ya pekee na haina gharama yoyote kujiunga, mteja anapata nafasi ya kushinda kutokana na matumizi yake ya kila siku. Wakazi wa Arusha kesho wanapata nafasi ya kuyashuhudia magari haya yakitembea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha na tutawapatia wateja wetu nafasi ya kununua line, kujisajili na kupata huduma zetu nyingi na kuwawezesha kujiunga na vifurushi vya yatosha ili waweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia
Hii ni nafasi ya pekee kwako mkazi wa Arusha kuchangamkia zawadi hii nono kwa kujiunga kwenye vifurushi vya yatosha sasa aliongeza Majwala
Airtel yatosha Zaidi ni promosheni yenye lengo la kuwazawadia wateja wake  nchini nzima ambapo kila siku Airtel itatoa Toyota IST moja kwa mshindi wa siku.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »