Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa rai kwa wakulima na wafugaji wote nchini kujikubali ni Watanzania

February 08, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akivunja Bunge. bu2Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Christopher Ole Sendeka, akijibu hoja za wabunge kuhitimisha mjadala.Kamati hiyo iliundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Aridhi, Kilimo, Mifugo,Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.
bu3 
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni Mstaafu John Chiligati, akichangia hoja.
Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, akichangioa taarifa ya kamati teule. bu5 
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Sabrina Sungura aichangia hoja.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman akichangia taarifa. bu7 
Wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya mkutano wa Bunge kuvunjwa. bu8 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.
bu9Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata.
bu10 
Baadhi ya wafugaji waliohudhuria Bungeni wakizaungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
……………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote bila kuvunja sheria.
Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji.
“Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema Pinda
Aliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha.
Hata hivyo Waziri Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko.
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha.
Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili.
“Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »