Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu)
akisalimiana na Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya
kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha
alipoenda kuzindua mradi wa BEYOND 2015 hivi karibuni.
Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu)
akisikiliza maelezo mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali la DSW
Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara
baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru Munasa
jijini Arusha juzi.Wa mwisho kushoto ni Mkuwa Wialaya ya Arumeru Mhe.
Nyirembe Munasa.
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw.
Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa
BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa
Shirikisho wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi
uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa
kipaumbele kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.la
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania Bibi. Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za
Vijana kutoka Wizara ya Afya, na Ustawi.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya
uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akifuarahi mara baada ya
kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini
Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo
watekelezaji wa mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na
Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester Mwanjesa aliyeshika kitabu.
Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiteta jambo na Mkurugenzia
wa DSW Tanzania(katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015 Bi.
Esther Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha
Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya Kimasai
kutoka kwa Mwanamke mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea
maonyesho ya biaadha zao katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa mradi wa
BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.
Picha ya pamoja
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mke wa Rais wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniella Schadt ametoa wito kwa jamii
kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye nyanja
mbalimbali za maendeleo.
Wito huo umetolewa juzi jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa
Ujerumani alipokuwa akizindua mradi wa utetezi na ushawishi wa jamii
katika kutoa vipaumbele katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana
ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo mradi huo unaratibiwa na Shirika
lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania.
Bibi. Daniela alisema kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika
sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana kwa kuwa duniani kote vijana
ndiyo nguvu kazi katika kuletea maendeleo ya taifa lolote lile.
‘Tunapaswa kuweka mkazo kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye
yanaanza kuanzia sasa, tuweke mkazo katika Elimu na Afya kwa vijana
wetu ili waeze kutambua fursa na kuzitumia.’’ Alisema Bibi. Daniela.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga
amesema kuwa ni wao kama asasi ya kirai wanashirikia na Serikali katika
kuhakikisha utekelezaji wa sera zinazohusu vijana nchini zinaleta tija
Owaga ameongeza kuwa Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa
kwa kuwa na Sera na miongozo mbalimbali inayohusu vijana kama vile Sera
ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inayotoa fursa kwa kijana
kujitambua.
Aidha Owaga aliongeza kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao
umezinduliwa na Mke wa Rais wa UjerumaniBibi. Daniela Schadt umelenga
kuongeza ushawishi na hamasa kwa washirika wa maendeleo ili kutoka
kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya Elimu , Afya ya Uzazi na
Ajira kwa vijana.
Akizungumzia mikakati na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa
Muhamasishaji na Mawasiliano Bi. Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo
utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika mikoa yote nchini ambapo mijadala
mbalimbali itakuwa ikifanyika ili kuongeza hamasa ya uashawishi
utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana hususan katika nyanja za
Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Mradi huu wa BEYOND 2015 ambao ni kifupi cha maneno Building
Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post 2015
Development umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya
kumalizika kwa muda wa Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.
EmoticonEmoticon